Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Agnes Kayola, amefanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed, katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa iliyopo mjini Songea.
Katika mazungumzo hayo, Balozi Kayola amesema ziara yake mkoani Ruvuma inalenga kujionea fursa zilizopo na namna zinavyoweza kuimarisha uchumi wa Tanzania na Malawi.
Pamoja na mambo mengine Balozi Kayola amesema Malawi huzalisha tani 200,000 za soya huku kiwanda cha Bakresa kikihitaji tani 800,000, na ukosefu wa ngano umekuwa ukisababisha kusimama kwa uzalishaji, hivyo ni fursa kwa wafanyabiashara wa nchi hizi kuwekeza.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brig. Jen. Ahmed Abbas, amesema Ruvuma ina fursa nyingi zinazohitaji wawekezaji, ikiwemo viwanda vya uchakataji wa mazao, ujenzi wa maghala, uchimbaji madini na uvuvi katika Ziwa Nyasa, akisisitiza kuwa uwekezaji huo utaleta maendeleo makubwa kwa mkoa na Taifa kwa ujumla.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.