Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma imepokea pikipiki 50 mpya kwa ajili ya maafisa ugani wa Programu ya BBT Korosho zikiwa ni silaha mpya ya kuimarisha uzalishaji na ubora wa zao la korosho kuanzia msimu wa 2025/2026.
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mhe. Denis Masanja, amesema pikipiki hizo ni sehemu ya mkakati kabambe wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuwafikia wakulima kwa urahisi na kuongeza tija katika kilimo.
“Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuona thamani ya watendaji na wakulima wetu. Pikipiki hizi zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa – kuongeza uzalishaji wa korosho, uti wa mgongo wa uchumi wa Tunduru,” alisema Masanja.
Shauri Makiwa, Meneja wa Bodi ya Korosho Tanzania – Tawi la Tunduru, amesema tayari maafisa 50 waliopangwa kata zote wameanza kushughulikia changamoto sugu kama matumizi ya viuatilifu na elimu ya kitaalamu kwa wakulima.
Pascal Kaguo, mmoja wa maafisa waliopokea pikipiki hizo, amesema hatua hiyo ni ukombozi mkubwa:
“Tumekuwa tukikumbwa na changamoto ya usafiri kwa muda mrefu. Sasa tutawafikia wakulima kwa haraka na kutoa huduma bora zaidi.”
Serikali inalenga kuvuka uzalishaji wa tani 700,000 za korosho kwa mwaka, lengo lililowekwa kupitia Ilani ya CCM 2020 – na sasa msingi wa mafanikio hayo umeanza kujengwa Tunduru!
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.