Mgombea mwenza wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi, ameahidi kuwaletea wananchi wa Wilaya ya Nyasa maendeleo makubwa kupitia sera za chama hicho.
Akizungumza katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Lituhi, wilayani Nyasa, Dkt. Nchimbi ameeleza dhamira ya serikali ya CCM ya kuboresha maisha ya wananchi kwa kuwekeza katika sekta mbalimbali muhimu.
Dkt. Nchimbi ameahidi kuendelea kuboresha Hospitali ya Wilaya ya Nyasa kwa kuipatia vifaa tiba vya kisasa, kuongeza majengo na idadi ya madaktari. Pia ameeleza mpango wa kujenga zahanati mpya 10 na vituo vya afya sita, ikiwemo kituo katika eneo la Lituhi, ili kuhakikisha huduma za afya zinapatikana kwa wananchi kwa urahisi na ubora zaidi.
Katika sekta ya elimu, ameeleza kuwa CCM imepanga kujenga shule mpya za msingi tisa na sekondari sita. Vilevile, kutajengwa madarasa mapya 210 kwa shule zilizopo na maabara 18 za kisayansi ili kuwasaidia wanafunzi kupata maarifa ya kina, hususan katika masomo ya sayansi.
Akizungumzia upatikanaji wa maji safi na salama, Dkt. Nchimbi amesema serikali ya CCM inalenga kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji kutoka asilimia 68 hadi kufikia asilimia 90 ambapo ameeleza kuwa hilo litatekelezwa kupitia miradi mikubwa ya maji inayotarajiwa kujengwa ili kuondoa changamoto ya maji.
Dkt. Nchimbi amesema katika sekta ya miundombinu, serikali cha chama hicho imepanga kujenga barabara kwa kiwango cha lami katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo ikiwemo barabara ya Mbambabay–Liuli–Lituhi yenye urefu wa kilomita 112, pamoja na kukamilisha barabara ya Kitai–Lituhi yenye urefu wa kilomita 93.
Ameongeza kuwa stendi ya kisasa itajengwa eneo la Kilosa ili kuboresha miundombinu ya usafiri katika wilaya hiyo na na wananchi wake kwa ujumla
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.