Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Makondo, amefurahishwa na elimu bunifu inayotolewa katika banda la Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, ambapo wataalam wa kilimo, mifugo, uvuvi na usindikaji wanatoa mafunzo ya vitendo yanayolenga kuongeza tija kwa wakulima na wajasiriamali.
Akizungumza baada ya kupokelewa na Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Pasifiki Mhapa, Makondo amesisitiza umuhimu wa elimu hii kwa maendeleo ya kaya na Taifa, akihimiza wakulima kujiunga na vyama kama Tanzania Mango Growers Association ili kupata masoko ya uhakika kwa matunda mengi kama embe yanayozalishwa Nyasa.
Pia amehamasisha ubunifu katika vifungashio vya bidhaa ili kuvutia masoko ya ndani na ya nje huku akipongeza vikundi vya wanawake na vijana wanaonufaika na mikopo ya asilimia 10 kwa kuongeza thamani ya mazao kwa kutengeneza bidhaa kama keki, tambi, maandazi na mikate badala ya kuuza mihogo ghafi.
Kauli mbiu ya mwaka huu: “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.”
#Nanenane2025 #RuvumaInawezekana #NyasaInang’ara #KilimoBora #MifugoNaUvuvi #MaryMakondo #RuvumaDigital #VijanaNaUbunifu
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.