Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma limeidhinisha rasimu ya bajeti ya zaidi shilingi bilioni 34.5 kwa mwaka wa fedha 2026/2027, hatua inayotarajiwa kuchochea kasi ya maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi kuanzia Julai 2026 hadi Juni 2027.Uamuzi huo umefikiwa , katika kikao maalum kilichoongozwa na Makamu Mwenyekiti Mh. Simon Kapinga, huku viongozi wakisisitiza kuwa bajeti hiyo inalenga matokeo yanayoonekana kwa jamii.
Akiwasilisha rasimu hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Idara ya Mipango, Bw. Venatus L. Venatus amesema mpango huo umejikita katika ustawi wa kijamii na kiuchumi kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya 2050, mpango mkakati wa Halmashauri pamoja na miongozo ya Serikali.Vipaumbele vikuu ni pamoja na:• Matumizi ya TEHAMA kuimarisha uwazi na uwajibikaji• Kuboresha huduma za jamii• Kuendeleza miundombinu endelevu na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi• Kuimarisha utawala bora na usimamizi wa fedha za ummaMapato yatatokana na vyanzo vya ndani, ruzuku ya Serikali Kuu na michango ya wadau wa maendeleo.Mkurugenzi Mtendaji Elizabeth Gumbo, amesisitiza kuwa bajeti hiyo itaongeza ufanisi wa miradi na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kwa wakati.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.