Maandalizi ya kumpokea Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, yamekamilika kwa kishindo mkoani Ruvuma.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Komred Oddo Mwisho, amethibitisha leo Septemba 20 baada ya kukagua maandalizi akiwa ameambatana na Mgombea Mwenza, Dkt. Emmanuel John Nchimbi.
Dkt. Samia atawasili kesho Septemba 21 kupitia Uwanja wa Ndege wa Songea, na kupokewa na viongozi wa chama pamoja na maelfu ya wananchi.
Ziara yake itaanzia Nyasa, akihutubia Mbinga na kufanya mkutano mkubwa wa kampeni Mbamba Bay.
Septemba 22 atazungumza na wakazi wa Songea katika viwanja vya VETA – Msamala, kisha kuelekea Namtumbo na Tunduru.
Septemba 23 ataendelea na kampeni zake mkoani Mtwara.

Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.