Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas, amekabidhi magari 24 mapya yaliyotolewa na Serikali kwa Jeshi la Polisi mkoani humo.
Hafla hiyo imefanyika katika viunga vya ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, ambapo Mkuu wa Mkoa amewataka askari kutumia magari hayo kwa umakini mkubwa na kuyafanyia matengenezo ya mara kwa mara ili yadumu na kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii.
“Magari haya yatapunguza kwa kiwango kikubwa changamoto za usafiri wa askari katika majukumu ya kila siku. Ni wajibu wenu kuyatunza na kuyatumia kwa weledi, utii na nidhamu, kwa sababu vitendea kazi hivi vipo kwa ajili ya kulinda raia na mali zao,” alisisitiza Abbas.
Aidha, Mkuu wa Mkoa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kulijali Jeshi la Polisi na kuwapatia vitendea kazi vinavyorahisisha utendaji wao.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Marco Chilya, ameishukuru Serikali na uongozi wa Jeshi la Polisi nchini, akisema magari hayo ni msaada mkubwa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu na yataimarisha zaidi ulinzi na usalama wa wananchi wema na mali zao.

Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.