Mgombea urais kupitia Chama cha MAKINI, Coaster Kibonde, akiwa na mgombea mwenza Azza Haji Suleiman, wamefanya ziara ya kampeni katika Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma, kunadi sera zao na dira yao ya uongozi kuelekea uchaguzi mkuu.
Katika hotuba yake kwa wakazi wa Songea, Kibonde amebainisha maeneo matatu ya kipaumbele ambayo serikali yake itayapa uzito endapo atachaguliwa akitaja elimu bora, kilimo chenye tija, na huduma za afya za uhakika, akisisitiza kuwa kushughulikia sekta hizo tatu kwa haraka kutaimarisha uchumi wa Tanzania na kuleta manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi.
Miongoni mwa mikakati aliyoainisha ni mpango wa kugawa hekari tano kwa kila kijana mwenye umri wa miaka 21 hadi 35, kama njia ya kuwawezesha kiuchumi, pia ameahidi kuimarisha miundombinu ya elimu na kuboresha mazingira ya kujifunzia.
Kwa upande wa afya, Kibonde ameeleza endapo atachaguliwa dhamira ya serikali yake ni kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana kwa watu wote.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.