MIAMBA ya kusini mwa Tanzania imeifungulia dunia ukurasa mpya wa historia ya uhai. Bonde la Ruhuhu mkoani Ruvuma limebainika kuwa chimbuko la baadhi ya mijusi wakongwe zaidi kuwahi kuishi duniani, wenye umri wa zaidi ya miaka milioni 240 kabla hata dinosaurs hawajatwaa dunia.
Masalia ya aina tatu za viumbe wa kale; *Ruhuhuaria, Ruhuhuensis* na *Ruhuhucerberus*, yamegunduliwa ndani ya Pori la Akiba la Litumbandyosi wilayani Mbinga mkoani Ruvuma Wataalamu wa kimataifa wanaeleza viumbe hao walikuwa sehemu ya kundi la archosaurs, chimbuko la mamba, ndege na hatimaye dinosaurs, hatua inayojaza pengo kubwa la kimageuzi duniani.
Ugunduzi huu unaibadili Ruvuma kuwa kitovu kipya cha utalii wa akiolojia Afrika Mashariki, sambamba na urithi wa Tendaguru wa Lindi. Serikali inaona fursa ya kuongeza watalii endapo miundombinu na matangazo ya kimataifa yataimarishwa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.