Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Mheshimiwa Reuben Kwagilwa, amesema ameridhishwa na maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Utiri–Mahande katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga, mkoani Ruvuma.
Akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo, Mheshimiwa Kwagilwa amekagua barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 16 na kumuelekeza mkandarasi kuongeza idadi ya wafanyakazi, vifaa na muda wa kazi pindi mvua zitakapopungua, ili mradi ukamilike kwa wakati na kuwanufaisha wananchi.
Amesisitiza kuwa miradi ya kimkakati kama ujenzi wa barabara hiyo lazima isisimamiwe kwa umakini ili iwe chachu ya maendeleo ya wananchi.
Mhe. Kwagilwa ameongeza kuwa barabara hiyo itarahisisha shughuli za kiuchumi, hususan usafirishaji wa mazao mbalimbali yanayozalishwa katika maeneo ya Mbinga na hivyo kuchangia katika kukuza uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake, Meneja wa TARURA Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Silivester Chinengo, amesema mradi huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 16 umefikia asilimia 69 ya utekelezaji na unatarajiwa kukamilika ifikapo Mei 29, 2026.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.