Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma ni hazina ya historia ya ukombozi wa Tanganyika. Katika kitongoji cha Mikulumo, kata ya Luegu, ndipo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alijificha Novemba 24–25, 1955, akiwakimbia askari wa kikoloni waliokuwa wakimtafuta kwa udi na uvumba.
Miongoni mwa mashujaa waliohatarisha maisha yao kumlinda, leo hii amebaki mzee Maulid Hassan (90) pekee, kijana wa miaka 20 wakati huo, aliyemficha Mwalimu kwenye vihenge vya chakula vya baba yake. Kwa siku nzima walishirikiana ugali wa ulezi na kuku, huku Mwalimu akizungumza kwa ari kubwa kuhusu Tanganyika kupata Uhuru.
Serikali sasa imeboresha mnara wa kumbukumbu ulipojificha Nyerere, ili kulinda urithi huu muhimu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Hapa ndipo historia ya Uhuru ilipoandikwa kwa ujasiri wa vijana na hekima ya kizazi kilichojitoa kwa ajili ya Taifa.

Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.