Mradi mkubwa wa kuboresha huduma ya maji safi katika Mji wa Mbinga, mkoani Ruvuma, unaotekelezwa na Serikali kupitia MBIUWASA, umefikia asilimia 64 ya utekelezaji!
Mkurugenzi Mtendaji wa MBIUWASA Mhandisi Yonas Ndomba anasema Mradi huu, unaotekelezwa na Ngogo Engineering Ltd, unahusisha ujenzi wa vyanzo viwili vyenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya lita milioni 1.6 za maji kwa siku, matenki manne yenye ujazo wa lita 525,000, na mtandao wa mabomba wa kilomita 57.
Mradi unatarajia kuhudumia zaidi ya wakazi 60,000 wa kata nane, mradi huu utaongeza upatikanaji wa maji kutoka asilimia 69 hadi 90 kufikia Desemba mwaka huu .
Wananchi wamesifu jitihada za Serikali na kuomba kasi iongezwe ili kero ya mgao wa maji iishe kabisa. “Tunashukuru kwa hatua hii, tunaona mwanga mpya wa maendeleo,” amesema Joyce Kapinga, mkazi wa Mbinga.

Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.