Katika hali ya kuvutia na isiyo ya kawaida, Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa imechukua maonesho ya Nanenane 2025 kwa kasi ya kipekee—kwa kuamua kuleta Ziwa Nyasa hadi ndani ya mabanda ya maonesho ya kitaifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya John Mwakangale, Jijini Mbeya!
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanavua Mlindoko, amesimama kidete kuipongeza Nyasa kwa kuwa kinara wa ubunifu, tofauti kabisa na mabanda mengine yenye bidhaa zinazofanana kama asali na vipando. “Huu ni ubunifu halisi – siyo kila banda kuja na bidhaa zilezile,” amesema Mhe. Mlindoko huku akisisitiza kuwa mabanda mengi yanakosa mvuto kwa watazamaji kutokana na kurudia vitu.
Mhe. Mlindoko amesifu hatua ya Nyasa kuonyesha Ziwa Nyasa kwa kutumia teknolojia ya kuvutia, ikiwemo:
• Elimu ya Uvuvi kwa njia ya vizimba,
• Ufugaji wa Samaki wa Mapambo na Dagaa,
• Na kuhamasisha uhifadhi wa mazingira ya ziwa kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
, ametoa wito kwa Halmashauri ya Nyasa kuendeleza kampeni ya kutangaza Ziwa Nyasa kupitia vyombo vya habari ndani na nje ya nchi, huku akilitaja ziwa hilo kama hazina ya utalii, samaki wa chakula na mapambo.
Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyasa, Ndugu Salum Ismail, amesisitiza dhamira ya halmashauri hiyo kufikisha elimu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa wananchi ili kuongeza kipato na kuinua pato la Taifa.
Maonesho ya Nanenane Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yanahusisha mikoa saba: Ruvuma, Katavi, Mbeya, Njombe, Iringa, Songwe na Rukwa.
Kaulimbiu ya 2025: “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.