Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa maono na uwekezaji mkubwa katika sekta ya kilimo, akisema matokeo chanya yanaonekana wazi kupitia uzalishaji mkubwa wa mazao mkoani humo.
Akihitimisha maonesho ya Nanenane ngazi ya mkoa katika Viwanja vya Amanimakoro, wilayani Mbinga, Kanali Ahmed alisema Mkoa wa Ruvuma umeendelea kuongoza kitaifa katika uzalishaji wa mazao ya chakula kwa miaka sita mfululizo, na katika msimu wa kilimo wa mwaka huu umezalisha zaidi ya tani milioni mbili za mazao mbalimbali.
Alibainisha kuwa mafanikio hayo yanachangiwa na mwamko wa wananchi, hali nzuri ya hewa, upatikanaji wa pembejeo za ruzuku na uwezeshaji wa vitendea kazi kwa maafisa ugani.
Aidha, alieleza kuwa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa matumizi ya mbolea nchini, ikitumia zaidi ya tani 100,000 msimu wa 2024/2025.
Amewahimiza wananchi wote kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa kuchagua Madiwani, Wabunge na Rais mwezi Oktoba 2025 ili kuweza kupata viongozi watakaoendelea kutuletea maendeleo katika sekta ya kilimo pamoja na sekta zingine za kiuchumi.

Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.