RUVUMA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA IDARA YA UHAMIAJI
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mheshimiwa Kapenjama Ndile, amesema Serikali ya Mkoa wa Ruvuma itaendelea kushirikiana kwa karibu na Idara ya Uhamiaji ili kuimarisha usalama wa mkoa na taifa kwa ujumla.
Akizungumza na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed, Mheshimiwa Ndile ameeleza kuwa Idara ya Uhamiaji imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kudumisha uhusiano na utulivu katika mipaka ya Tanzania na nchi jirani za Malawi na Msumbiji.
Amesisitiza kuwa juhudi hizo zimekuwa chachu ya ustawi wa biashara na ushirikiano wa kijamii na kiusalama kati ya mataifa hayo.
Mheshimiwa Ndile ameongeza kuwa Serikali ya Mkoa wa Ruvuma inatambua mchango wa Idara ya Uhamiaji katika kulinda mipaka na kuhakikisha wananchi wanaendelea kunufaika na fursa za kiuchumi zinazojitokeza kutokana na usalama wa mipaka.
Kwa upande wake, Kamishna Jenerali Dkt. Anna Makakala, amesema ushirikiano mkubwa wanaoupata kutoka Serikali ya Mkoa wa Ruvuma umekuwa nguzo muhimu ya mafanikio ya kazi za Idara ya Uhamiaji. Akibainisha kuwa msaada huo unawapa nguvu na kuimarisha utekelezaji wa majukumu yao kwa ufanisi mkubwa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.