SEKONDARI ya wasichana ya Dkt Samia Suluhu Hassan iliyojengwa katika kata ya Rwinga Wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma kwa gharama ya shilingi bilioni nne imeanza kuchukua wanafunzi wa kidato cha Tano mwaka huu.
Mkuu wa shule hiyo mpya ya Mkoa wa Ruvuma MWL.Dafrosa Chilumba amesema serikali imewapangia wanafunzi 249 wa kidato cha tano na kwamba sekondari hiyo ina uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 1000 watakaokuwa wanasoma kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita.
Sekondari ya wasichana ya Dkt Samia Suluhu Hassan Namtumbo mkoani Ruvuma ni miongoni mwa sekondari mpya kumi za wasichana za mikoa zilizojengwa na serikali ya Awamu ya Sita
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.