Serikali imepiga hatua kubwa katika kuboresha huduma za afya vijijini,Kupitia Wizara ya Afya, zaidi ya shilingi milioni 891 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa vituo vipya vya afya viwili katika Kata za Peramiho na Mpandangindo, Halmashauri ya Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma — hatua itakayowanufaisha wananchi zaidi ya 23,800.
Fedha hizo zinajumuisha milioni 641.6 kwa kituo cha afya Peramiho na milioni 250 kwa kituo cha Mpandangindo.
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Elizabeth Gumbo, amesema fedha hizo zinaakisi dhamira ya Serikali kuhakikisha kila kata inapata kituo cha afya chenye huduma muhimu.
Kwa upande wake, Dkt. Geofrey Kihaule, Mganga Mkuu wa Wilaya, amesema miradi hiyo itapunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya ya Songea na kuongeza kasi ya huduma hasa kwa akina mama wajawazito, watoto .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.