Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mkoani Ruvuma Denis Masanja, amezindua ugawaji wa madawati 939 mapya kwa shule za msingi na sekondari ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, katika hatua inayolenga kumaliza uhaba wa viti vya kujifunzia na kuboresha ufaulu.
Mradi huo umegharimu Sh. milioni 103.3, fedha zilizotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri, huku madawati yakitengenezwa kwa ubora unaostahimili matumizi ya muda mrefu.
Masanja amesema uwekezaji huu ni sehemu ya mkakati wa serikali kuboresha mazingira ya kujifunza, kuongeza hadhi ya elimu ya wilaya, na kuonesha namna usimamizi makini wa mapato ya ndani unavyoweza kuleta mabadiliko ya moja kwa moja kwa jamii..
Madawati haya yanatarajiwa kupunguza msongamano wa kukaa chini, kuongeza morali ya wanafunzi na walimu, na kuimarisha viwango vya kimataifa vya elimu ya msingi na sekondari wilayani humo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.