Oktoba 14 ni maadhimisho ya NyerereDay, siri nzito imefichuka kutoka kijiji kidogo cha Luegu, wilayani Namtumbo, mkoani Ruvuma ,mahali ambapo mwaka 1955, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alijificha kwa siku mbili akitoroka mikono ya wakoloni waliokuwa wakimtafuta usiku na mchana.
Ndani ya vihenge vya nafaka, si chakula pekee kilichohifadhiwa bali ndoto ya uhuru wa Tanganyika. Wakulima wa kawaida, akiwemo kijana Maulid Hassan Mang’unyuka ambaye hivi sasa ana miaka 90, waligeuka ngao ya taifa kwa kumficha Mwalimu na kumlisha ugali wa ulezi huku wakipanga mustakabali wa taifa jipya.
Leo, eneo hilo limegeuka urithi wa kihistoria,likiwa na mnara wa kumbukumbu, kivutio cha watalii na kituo cha kujifunza kwa vijana wanaotaka kuelewa mizizi ya uhuru.
Mzee Mang’unyuka anasema kwa fahari, “Kama asingejificha hapa, labda historia ya Tanganyika ingekuwa tofauti.”
Kijiji cha Luegu ni ishara ya ujasiri, mshikamano na imani. Ndani ya vihenge hivyo vilizaliwa ndoto ya taifa lenye amani, umoja na heshima.

Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.