Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Seikali za Mitaa (OWM- TAMISEMI) imekamilisha maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa elimu ya awali, Darasa la Kwanza na Kidato cha Kwanza kwa mwaka 2026 na kuwataka Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, viongozi wa Halmashauri kushirikiana na wadau wa elimu ili kuhakikisha wanafunzi wote wakiwemo wenye mahitaji maalum, wanaanza masomo Januari 13, 2026 bila vikwazo vyovyote.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini OWM -TAMISEMI Bi. Roida Andusamile ambaye amebainisha kuwa zaidi ya Shilingi Bilioni 196.7 zimetumika kujenga shule mpya, madarasa ya elimu ya awali, msingi na maalum pamoja na matundu ya vyoo.
Aidha, zaidi ya Shilingi Bilioni 14.1 zimetumika kuandaa miundombinu itakayowezesha shughuli za ufundishaji na ujifunzaji katika shule za msingi.
Amesema Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya elimu kupitia ujenzi wa shule mpya, madarasa, vyoo, maabara, shule za amali na ununuzi wa vifaa vya TEHAMA, ambapo zaidi ya Shilingi Bilioni 283 zimetumika.
Kwa upande wa elimu ya sekondari, Bi. Andusamile amesema Serikali ilitoa zaidi ya Shilingi Bilioni 28.4 kama ruzuku ya uendeshaji wa shule hizo, ili ziweze kuwahudumia wanafunzi 937,581, wakiwemo wenye mahitaji maalum 3,228 ambao walipangiwa shule kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa Kidato cha Kwanza yaliyotangazwa Desemba 04, 2025.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.