Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) Dkt. Thomas Bwana, akiwa na Maafisa kutoka TARI Makao Makuu, amefanya ziara Wilayani Tunduru. Ziara hiyo ilianzia katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ambako walijadili masuala muhimu ya maendeleo ya kilimo kupitia kituo cha TARI Tunduru, tawi la TARI Naliendele.
TARI Tunduru imeendelea kung’ara katika tafiti za mazao ya Korosho, Ufuta na Mbaazi, ambayo ni uti wa mgongo wa uchumi wa wananchi wa Tunduru. Mkuu wa Wilaya, Mhe. Denis G. Masanja, amepongeza juhudi hizo na kuiomba TARI kuongeza tafiti za mbegu bora za mazao ya chakula na mbogamboga zinazostahimili hali ya hewa ya eneo hilo.
Aidha, ameitaka TARI kushirikiana na TFRA kuhakikisha upatikanaji wa mbolea unarahisishwa ili kuinua uzalishaji na kipato cha wakulima wa Tunduru.
Kilimo Bora, Maisha Bora – TARI inaendelea kuwa nguzo ya maendeleo ya kilimo Tanzania!

Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.