Watoto wachanga wanapaswa kuanza kunyonyeshwa maziwa ya mama ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa ili maziwa yaanze kutoka mapema.
Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) wanaeleza kuwa inashauriwa mara baada ya kujifungua mama na mtoto wagusane ngozi kwa ngozi ili kusaidia maziwa kutoka na kuongeza uhusiano kati ya mama na mtoto. Ni muhimu kwa mtoto kuwekwa kwenye titi ili aanze kunyonya maziwa ya mama.
Mama na mtoto wasitenganishwe, wawe pamoja muda wote, ila wanaweza kutenganishwa kwa ushauri wa daktari ikiwa kuna tatizo litakalomuathiri mtoto akiwa na mama yake mfano ugonjwa wa mtoto au mama.
Kumnyonyesha mtoto ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa kuna faida nyingi ikiwemo:
Umuhimu wa maziwa ya njano kwa mtoto
Maziwa ya njano ni maziwa ya mwanzo, mazito yenye rangi ya njano ambayo hutoka siku chache za mwanzo baada ya kujifungua. Maziwa haya ni chakula kamili chenye virutubishi vingi, na pia yanatoa kinga maalum dhidi ya maradhi.
Aidha maziwa ya njano humsaidia mtoto kutoa kinyesi cha mwanzo chenye rangi ya kijani au nyeusi ambacho humfanya mtoto aumwe tumbo siku za mwanzo kama hatanyonya.
Virutubisho vilivyomo kwenye maziwa ya mama
Maji 87%
Wanga 7%
Mafuta 4%
Protin 1%
Vingine 1% (Vitamini, madini, kingamwili, vimeng'enya, Kiinitete)
Kunyonyesha kunampunguza hatari ya magonjwa kwa mtoto, mama
Mtoto anaponyonya inaweza kumsaidia kupunguza hatari ya kupata magonjwa yafuatayo:
Pumu
Unene kupita kiasi
Aina 1 ya kisukari
Ugonjwa mkali wa kupumua kwa chini
Maambukizi ya sikio
Ugonjwa wa kifo cha ghafla cha watoto wachanga (SIDS)
Maambukizi ya njia ya utumbo
Mama anaponyonyesha inaweza kupunguza hatari ya kupata magonjwa yafuatayo:
Shinikizo la damu
Aina ya 2 ya kisukari
Saratani ya ovari
Saratani ya matiti
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.