Upatikanaji wa umeme mkoani Ruvuma umefikia hatua ya kihistoria, baada ya Mkoa kuunganishwa kikamilifu na Gridi ya Taifa, hatua inayobadilisha maisha ya wananchi na kuongeza kasi ya maendeleo katika Wilaya zote.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brig. Jen. Ahmed Abbas Ahmed, vijiji vyote 551 sasa vina umeme sawa na asilimia 100 ya vijiji vya mkoa huo. Aidha, vitongoji 1,975 kati ya 3,693 vimepatiwa huduma hiyo, ikiwa ni asilimia 53.5 ya jumla ya vitongoji.
Ruvuma imekuwa miongoni mwa mikoa inayofaidika na ujenzi wa gridi imara nchini, ikijumuisha upanuzi wa vituo vya kupozea umeme katika kila Wilaya.
Kwa sasa, mradi unaotekelezwa na Kalpataru Projects International Limited kutoka India kwa gharama ya Sh bilioni 150.78, wenye urefu wa km 214.5, umefikia asilimia 50.6 na unajumuisha ujenzi wa kituo kipya cha kupozea umeme Tunduru.
Wakati huohuo, maandalizi ya ujenzi wa njia ya umeme wa KV 220 Songea–Mbinga yanaendelea, hatua itakayomaliza kabisa changamoto za kukatika kwa umeme na kuimarisha uchumi wa mkoa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.