Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, amesema changamoto kubwa inayowakabili vijana nchini ni idadi yao kubwa ikilinganishwa na fursa chache zilizopo.
Akizungumza na viongozi mbalimbali katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, amesisitiza kuwa ni wajibu wa serikali na viongozi kuhakikisha vijana wanapewa nafasi ya kusikilizwa, kueleweka na kuandaliwa mazingira mazuri ya kufanikisha maisha yao.
Mhe. Nanauka amesema ziara yake inalenga kuzungumza na vijana katika maeneo mbalimbali nchini. Akibainisha kuwa lengo la ziara hiyo ni kusikiliza mawazo ya vijana na kuangalia namna bora ya kutatua changamoto walizonazo.
Ameeleza kuwa vijana wengi kwa sasa wamejiajiri kupitia bodaboda na bajaji, lakini ili kupunguza tatizo la ajira ni muhimu kuwaelekeza kwenye viwanda na shughuli za kuongeza thamani ili kuinua maisha yao.
Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Gasper Makondo, amesema mkoa umeweka mkakati shirikishi wa kuinua maisha ya vijana ambapo amebainisha kuwa hatua hizo ni pamoja na kuwatafutia maeneo ya ufugaji nyuki, kilimo cha miti, pamoja na kuwasaidia kupata maeneo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.