WADAU wa sekta ya afya na maendeleo wilayani Songea mkoani Ruvuma wamepatiwa elimu ya utekelezaji wa Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Kikao cha kujengea uwezo wadau hao kimewakutanisha wataalam wa afya kutoka vituo vya huduma, watendaji wa kata na vijiji, pamoja na maafisa kilimo wa kata makundi yenye mchango wa moja kwa moja katika kutoa elimu kwa jamii.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea, Ndugu Mtela Mwampamba, akifungua kikao, amesema uelewa wa wananchi ndiyo “injini ya mafanikio” ya mpango huu.
Ameeleza kuwa bima ya afya ni ngao ya kiuchumi inayolinda familia dhidi ya gharama kubwa za matibabu .
Mwenyekiti wa Halmashauri, hiyo Mhe. George Ponera, amewataka washiriki kuwa mabalozi wa elimu hiyo kwenye maeneo yao ya kazi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.