Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wamepatiwa mafunzo ya mfumo wa manunuzi ya umma (NeST) yaliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Kanda ya Kusini.
Mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Songea Club mjini Songea yamelenga kuwajengea uwezo watumishi katika matumizi ya mfumo huo na kuhakikisha manunuzi yanafanyika kwa uwazi, ufanisi na kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa ili kulinda rasilimali za taifa.
Afisa Ununuzi kutoka PPRA Kanda ya Kusini, Ndg. Theophil Ngowi, amesema kuwa baada ya mafunzo hayo wanatarajia watumishi kutumia maarifa waliyopata, ikiwemo kuzingatia sheria, makatazo na matumizi ya mfumo wa NeST katika kufanikisha manunuzi ya umma.
Kwa upande wake, Afisa Ununuzi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Ndg. Patrick Mahema, amesema kuwa mafunzo hayo yamewajengea uwezo mpya utakaowasaidia katika utendaji wao wa kila siku. Amesisitiza kuwa mafunzo hayo yamewapa uelewa mpana na sasa wanaamini utendaji wa ofisi utaimarika zaidi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.