Katika kilele cha maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi, amesema serikali inajivunia mafanikio makubwa ya kihistoria yaliyochochea ukuaji wa uchumi, kuimarisha Muungano na kuboresha maisha ya wananchi.
Akihutubia taifa, jana Dk Mwinyi alisema amani na utulivu vimeendelea kudumishwa huku Mapinduzi yakizidi kuimarisha Muungano wa Tanzania kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hoja 15 za Muungano zimeondolewa na hati 13 za maamuzi kusainiwa.
Kiuchumi, Zanzibar imepiga hatua kubwa ambapo mwaka 2024 uchumi ulikua kwa asilimia 7.1 kutoka asilimia 1.3 mwaka 2020. Pato la taifa limefikia Sh trilioni 6.57, mapato ya serikali Sh trilioni 2.104, na mfumuko wa bei kudhibitiwa hadi asilimia 5. Uwekezaji umefikia miradi 1,657 yenye thamani ya dola bilioni 20.2.
Serikali pia imepanua ajira kwa vijana, kuimarisha utalii, kupambana na rushwa, kuboresha utumishi wa umma na kuimarisha mapambano dhidi ya umaskini kupitia TASAF na huduma za kisheria kwa wananchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.