Afisa Elimu Mkoa wa Ruvuma, Mwalimu Edith Mpinzile, ameweka bayana mikakati mbalimbali waliyopanga ili kuinua kiwango cha ufaulu katika mkoa huo.
Akizungumza katika mkutano wa wadau wa elimu uliofanyika katika ukumbi wa Chandamali mjini Songea, Mwalimu Mpinzile amesema wanahitaji suala la elimu kuzungumzwa katika kila mkutano zikiwemo habari za watoro, chakula, uwajibikaji wa kila mmoja, uandikishaji, hali ya kidato cha kwanza kuripoti shuleni na ufafanuzi wa umuhimu wa Elimu.
Mikakati mingine ni kufanya mazungumzo baina ya timu itakayoundwa na walimu ambao hawatimizi wajibu wao au wanaofanya vibaya zaidi katika ufaulu wa masomo ambapo mazungumzo hayo yatashirikisha wakuu wa shule na maafisa elimu wa kata husika ili waweze kueleza sababu zinazopelekea kutofanya vizuri.
Amebainisha kuwa wamependekeza timu hiyo iundwe na Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri, Mwenyekiti wa Halmashauri, Maafisa Elimu wote wawili, Afisa Utumishi, Mthibiti Ubora wa Shule, na Katibu wa TSC, lengo likiwa ni kuhakikisha wadau wote wanashirikishwa katika kuboresha elimu na sio kumuachia Afisa Elimu au mtaalamu wa elimu pekee.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.