JUMLA ya wanafunzi 1367 kati ya wanafunzi 2717 waliopangiwa kuanza kidato cha kwanza katika shule za sekondari za Serikali 15 Halmashauri ya Mji Mbinga mkoani Ruvuma wameripoti na kuanza masomo hadi kufikia Januari 20,2023.
Mwakilishi wa Afisa Elimu Sekondari katika Halmashauri hiyo Lucy Luwungo amesema idadi ya walioripoti ni sawa na asilimia 50.2 na kwamba wanatarajia hadi kufikia mwishoni mwa Januari zaidi ya asilimia 80 ya wanafunzi wa kidato cha kwanza watakuwa wameripoti.
Amesema Halmashauri ya Mbinga Mji pia imeisajiri sekondari mpya ya Lusonga ambayo serikali kupitia program ya SEQUIP ilitoa shilingi milioni 470 kutekeleza mradi huo.
Amesema shule imeanza na mikondo miwili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kuanzia Januari mwaka huu
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.