WAKALA wa barabara za mijini na vijijini(TARURA) Mkoa wa Ruvuma,kwa mwaka wa fedha 2024/2025 umeidhinishiwa katumia kiasi cha Sh.bilioni 22,194,409,504.77 kwa ajili ya kufanya matenengezo ya barabara zake.
Meneja wa TARURA Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Silvester Chinengo amesema ,kati ya fedha hizo kutoka Mfuko Mkuu wa Barabara ni Sh.bilioni 7,894,961,998.36 na mfuko mkuu wa serikali wa kila jimbo shilingi shilingi bilioni 4,500,000,000.00 ,fedha za tozo ya mafuta Sh.100 kwa lita ni Shilingi bilioni 9,799,447,506.41.
Chinengo amesema hayo kwenye hafla fupi ya utiaji saini mikataba ya matengenezo ya Barabara iliyoshuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed mjini Songea.
“mpaka sasa TARURA tumekamilisha manunuzi ya miradi 50 yenye gharama ya Sh.bilioni 14,19,607,702.00 ambapo jumla ya kilometa 1,079 za barabara zitafanyiwa matengenezo ya aina mbalimbali pamoja na ujenzi wa makalavati na madaraja”alisema Chinengo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema ,serikali kupitia TARURA itahakikisha inawalipa Wakandarasi fedha zao ili kuwajengea uwezo katika utekelezaji wa majukumu yao.
Ameziagiza Taasisi za serikali mkoani humo,kulipa madeni ya wakandarasi kwa wakati ili kuwaepusha wakandarasi kuingia kwenye migogoro mbalimbali ikiwemo kunyang'anywa na kuuziwa mali zao na taasisi za fedha kutokana na fedha walizokopa kama mitaji katika shughuli zao.
Amesisitiza kuwa ,serikali kupitia sekta ya mawasiliano ya barabara imejipanga kuona sekta ya barabara inaimarika ili kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji wa mazao kutoka shambani kwenda mijini kwa ajili ya kupata soko la uhakika.
Katika hatua nyingine Kanali Abbas,amezitaka Taasisi za Serikali mkoani humo, kuwapa kipaumbele wakandarasi wazawa na kutoa upendeleo kwa wanawake wanaofanya kazi za ukandarasi ili kuwajengea uwezo na kunufaika na fedha zinazotolewa
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Mary Makondo,amewataka watendaji wa TARURA kuwafuatilia kwa karibu wakandarasi ili miradi inayotekelezwa ikamilike kwa muda uliopangwa na kwa viwango vinavyohitajika.
Naye Mkuu wa TAKUKURU mkoani Ruvuma Hamza Mwenda amesema , TAKUKURU itahakikisha inafuatilia miradi yote iliyopangwa kutekelezwa ili kujiridhisha ubora wa miradi husika.
Mwakilishi wa Wakandarasi wa Mkoa wa Ruvuma Vales Urio kutoka Kampuni ya Ovans Contructions Ltd,ameishukuru serikali kwa kuendelea kuwaamini na kuwapa kazi za ujenzi wa miradi ya barabara na kuhaidi watekeleza miradi hiyo kwa ubora ili kuleta tija kwa mkoa na Taifa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.