Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeidhinisha kuanza kwa mradi mkubwa wa umwagiliaji katika Kijiji cha Nambarapi, Kata ya Masonya, Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma
.Mkandarasi aliyepewa dhamana ya kutekeleza mradi huu anatarajia kuanza kazi tarehe 29.07.2024, na mradi unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 18.
Makabidhiano ya mradi huu wenye thamani ya shilingi bilioni 6,314,477,066.00 baina ya Tume ya Taifa ya umwagiliaji na Mkandarasi yamefanyika kwa sherehe za hadhara katika kijiji cha Nambarapi, AMBAZO zimehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Simon Chacha.
Katika hotuba yake Chacha ameeleza umuhimu wa mradi huu katika kukuza uchumi wa wilaya na kuboresha maisha ya wananchi na kumtaka Mkandarasi aliyekabidhiwa mradi huu kutekeleza mradi kwa muda uliopangwa na kuzingatia ubora.
“Mradi huu ni ushahidi wa dhamira ya Serikali ya kuwekeza katika sekta ya kilimo na kuboresha maisha ya wananchi '',alisisitiza Mkuu wa Wilaya.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.