Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Mtela Mwampamba, amewataka Wananchi wa wilaya ya Songea kukata Bima ya Afya ili kuwa na uhakika wa matibabu na Afya zao.
Mwampamba ameyasema hayo wakati anazungumza kwenye Mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Peramiho uliofanyika katika vijiji vya Nakahuka na Morogoro kata ya Litisha.
“ Ndugu zangu wananchi, najua sasa wengi mmevuna mazao mna uwezo wa kukata Bima hata zile za 30,000 ambazo zinaweza kutibu watu sita. Hivyo nitoe wito kwa wananchi wote mjitahidi kuwa na Bima ya afya ili kujiwekea uhakika wa kupata matibabu wakati wote'',alisisitiza .
Mwampamba pia amewakumbusha wananchi kupata cheti cha kuzaliwa kupitia simu yako Simu janja ( Smart Phone) ili kupunguza safari za kwenda Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kufuata chet cha kuzaliwa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.