Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, mkoani Ruvuma Mhe. Kisare Makori, amekabidhi mahitaji muhimu kwa wafungwa wa Gereza la Kitai ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Thamani ya msaada huo ni zaidi ya shilingi milioni mbili.
Makabidhiano hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake katika Wilaya ya Mbinga. Hafla hiyo ilifanyika ndani ya ukumbi wa gereza hilo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Makori aliwapongeza wanawake wa Wilaya ya Mbinga kwa kutambua kundi hilo la wafungwa na kushiriki katika jitihada za kuwapatia msaada. Alisisitiza umuhimu wa kuwasaidia watu walioko magerezani ili kuboresha ustawi wao.
Msaada huo ulijumuisha buti 200 za kufanyia kazi, gunia moja la mchele, miche ya sabuni, sukari, mafuta, dawa za meno, na bidhaa nyingine muhimu kwa mahitaji ya kila siku.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wanaharakati wa haki za wanawake, pamoja na maafisa wa gereza, ambapo wote walionesha mshikamano katika kusaidia kundi hilo maalum.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.