Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma, Mhe. Ngollo Malenya, amewataka wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kuchagua viongozi makini na waadilifu badala ya wanaharakati katika uchaguzi wa viongozi wa chama hicho kwa kipindi cha mwaka 2025 hadi 2030.
Alisema kuwa uongozi bora ni msingi wa maendeleo ya walimu na sekta ya elimu kwa ujumla.
Akizungumza lwakati wa Mkutano Mkuu wa CWT wilayani Namtumbo, uliofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Malenya alisisitiza umuhimu wa viongozi wenye maadili, uwajibikaji, na ushirikiano mzuri na serikali.
Alisema viongozi hao wanapaswa kuwa tayari kushirikiana na serikali ili kutatua changamoto za walimu kwa njia ya busara na mazungumzo yenye tija.
“Ni muhimu kuchagua viongozi, si wanaharakati. Tunahitaji watu watakaoshirikiana na serikali kuhakikisha walimu wanapata haki zao kwa njia ya busara, hekima, na mazungumzo yenye tija,” alieleza Mhe. Malenya.
Mhe. Malenya pia alisisitiza umuhimu wa walimu na viongozi wao kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake za kuboresha sekta ya elimu.
Alisema kuwa serikali imeendelea kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika elimu, hivyo ni jukumu la walimu kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii, maarifa, na uzalendo ili kufanikisha azma hiyo.
Mkutano huo ulikuwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi wa viongozi wa CWT wilayani Namtumbo kwa kipindi cha mwaka 2025 hadi 2030. Ulijumuisha walimu kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari,.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.