Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Neema Maghembe anawakumbusha wazazi na walezi wote katika Halmashauri ya wilaya ya songea kuwa zoezi la uandikishaji wanafunzi wa darasa la awali na darasa la kwanza linaendelea katika shule zote ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea
Kufuatia mkakati wa uboreshaji wa Elimu wa mwaka 2022 uliazimia watoto wa awali na darasa la kwanza waandikishwe kuanzia tarehe 1 Octoba hadi tarehe 31 Disemba na utekelezaji wake umeanza rasmi mwaka huu wa 2023 ili ifikapo januari 2024 watoto waanze masomo kwa kuingia darasani.
Akizungumzia uandikishaji huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea amewaomba wazazi na walezi kutumia nafasi hii kwa sasa ili ifikapo Januari watoto waanze masomo na sio usajili tena. Amesema
“Kwa wazazi wote ambao wanaona kwamba watoto wao wamefikia umri wa kuanza shule basi wafike katika shule iliyopo jirani na yeye ili kumuandikisha mototo wake ambapo kwa darasa la awali umri ni miaka 5 hadi 6 na kwa darasa la kwanza umri ni miaka 7 hivyo natoa rai kwa wazazi na walezi wote muda ndio huu wa kuandikisha watoto wetu ili waanzekupata elimu”
“Pia natoa wito kwa viongozi wa Chama na Serikali, pamoja na taasisi za dini kufikisha ujumbe huu kila sehemu ambako wanahudumia wananchi na waumini wao ili watu wote waweze kufahamu kuhusiana na taarifa hii, vilevile kwa wale wazazi na walezi ambao wanaishi na watoto wenye ulemavu wowote ule wasiwafiche watoto hao majumbani kwao, kama wamefikia umri wa kuanza shule basi wawapeleke shuleni kuwaandikisha kwani mazingira ya kuwalea yapo na yanaruhusu” Alisema Ndg Neema M Maghembe Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Uandikishaji huu ulianza rasmi tarehe 1/10/ 2023 na unatarajiwa kukamilika tarehe 31/12/2023, kaulimbiu ya uandikishaji huu ni “KILA MTOTO ANAHAKI YA KUPATA ELIMU, HAKIKISHA UNAMUANDIKISHA”.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.