MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Chiza Marando amemsimamisha kazi tabibu wa Zahanati ya Marumba, Ignas Yustine Magomba, kufuatia kifo cha mwanamke mmoja, Zainabu Kazembe Boma, kilichotokea kijijini Marumba.
Uamuzi huo umechukuliwa baada ya familia ya marehemu kueleza kutoridhishwa na huduma alizopokea kutoka kwa tabibu huyo kabla ya kufariki dunia.
Malalamiko hayo yameenea kwenye mitandao ya kijamii, yakidai uzembe ulifanyika katika utoaji wa huduma za afya
Marando amesema uchunguzi wa kina unafanyika ili kubaini iwapo kulikuwa na ukiukwaji wa maadili ya kazi.
Amesisitiza kuwa hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayepatikana na hatia ya uzembe.
Amewataka wahudumu wa afya kutoa huduma kwa kuzingatia sheria, kanuni, na miongozo ya kazi.
Hata hivyo ametoa rai kwa , jamii kutoa taarifa mapema kwa mamlaka husika wanapokumbana na changamoto katika sekta ya afya.
Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, na marafiki wa marehemu kwa msiba huo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.