Mkuu Wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za kujenga miundombinu ya elimu ikiwemo shule,madarasa na ununuzi wa samani mbalimbali ambapo ametoa rai kwa wananchi kuwapuuza watu wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii kwa kutoa taarifa ambazo sio sahihi
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, amepongeza juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutoa fedha za ujenzi wa miundombinu ya shule za msingi na sekondari, hatua ambayo inatengeneza mazingira bora zaidi ya kujifunza kwa wanafunzi katika mkoa huo.
Katika uongozi wa serikali ya Awamu ya Sita, Mkoa wa Ruvuma unajivunia ongezeko la idadi ya shule, miundombinu bora, na mikakati ya kisasa ya maendeleo ya elimu.
Ongezeko la Shule na Miundombinu ya Elimu
Mkoa wa Ruvuma umeshuhudia ongezeko la shule za msingi kutoka 841 zilizokuwepo mwaka 2023 hadi shule 860 mwaka 2024, ikiwa ni sawa na asilimia 1.8.
Hii ni ishara ya maendeleo ya sekta ya elimu, ambapo shule za sekondari pia zimeongezeka kutoka shule 233 mwaka 2023 hadi kufikia shule 247 mwaka 2024.
Juhudi za Uboreshaji wa Miundombinu
Mkoa wa Ruvuma, kwa kushirikiana na wilaya zake, umeendelea na juhudi mbalimbali za kuhakikisha kwamba upungufu huu wa miundombinu unadhibitiwa.
Katika shule za sekondari mkoani Ruvuma, mahitaji ya vyumba vya madarasa yamepungua, huku Mkoa ukiwa na vyumba vya madarasa 2,341, ikiwa hakuna upungufu katika eneo la shule za sekondari.
Hata hivyo jitihada kubwa zinaendelea kufanywa na serikali kuhakikisha nyumba za walimu,matundu ya vyoo,vyumba vya maabara na mabweni yanaendelea kujengwa ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi
Vyuo vya Elimu ya Juu na Ufundi
Mkoa wa Ruvuma umeonesha mafanikio pia katika sekta ya elimu ya juu na ufundi ambapo Mkoa una vyuo vya Maendeleo ya Wananchi tisa, vyuo vya ufundi stadi (VETA) vitano, vyuo vya ualimu vitatu, na Chuo Kikuu kimoja.
Serikali pia inatekeleza ujenzi wa chuo cha ufundi kwa watu wenye ulemavu unaendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea, jambo linaloonesha ufanisi wa serikali katika kuhakikisha elimu inapatikana kwa watu wote, bila kujali changamoto zinazowakumba.
Ujenzi wa shule mpya, vyuo, na miundombinu mingine ya elimu ni ishara ya maendeleo endelevu na juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya Awamu ya Sita ya kuboresha miundombinu ya elimu katika Mkoa wa Ruvuma.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.