Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema hakuna mgonjwa anayesafirishwa kwa njia ya Pikipiki huku akiwa amewekwa kwenye tenga kupelekwa kupata huduma za afya katika Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma
Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo wakati akitoa salaam za Wizara kwenye mkutano wa hadhara wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na wananchi wa Tunduru uliofanyika kwenye uwanja wa Ccm mjini Tunduru.
Amesema ameona taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikionesha mgonjwa akisafirishwa kwenye Pikipiki huku akiwa kwenye tenga na kueleza kuwa hakuna magari ya kusafirishia wagonjwa jambo ambalo ni upotashaji.
“Napenda kukuthibitishia Mhe. Rais hapa Tunduru hakuna upungufu wa magari ya kubebea wagonjwa na kati ya Magari 535 tuliyoyakabidhi mwaka jana kwa muongozo wako Mhe. Rais hapa Tunduru walipata Magari mapya manne ya kubebea wagonjwa”‘alisisitiza
Amesema magari hayo yalipekwa kwenye Kituo cha Afya Nakapanya, Matemanga, Nalasi na Mchesi ambayo yanafanya kazi saa 24 na rufaa zote zinaratibiwa kwa utaratibu maalumu na sio kuchangisha wananchi.
Ameutaja utaratibu unaotumika kusafirisha wagonjwa ni kutumia magari ya kubebea wagonjwa (Ambulaces) na kwa kutumia madereva ngazi ya jamii waliosajiliwa wakati wa mfumo wa M-Mama ambapo mfumo huu unahusika na kusafirisha wakina mama wajawazito na watoto wachanga bila malipo yoyote.
Ameongeza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ina jumla ya madereva wa jamii 20 walioingia mikataba na Serikali; Hivyo taarifa hizi zipuuzwe kwani zinalengo la kuupotosha umma, kuleta taharuki kwa jamii na kuichafua Serikali.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.