HALMASHAURI ya Madaba Wilaya ya Songea wamefanya kikao cha Barala la Madiwa cha robo tatu ya mwaka na kuazimia kukamilisha miradi yote kabla ya kumaliza mwaka wa fedha 2021-2022.
Akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Songea katika Baraza Hilo Pololet Mgema amesema ifikapo Juni 30 ,2022 Miradi yote inayoendelea katika Halmashauri ya Madaba iwe imekamilika kwa asilimia miamoja na kuanza kutumika.
Amesema fedha za umma zitumike kwa mujibu wa Sheria na kwa malengo kusudiwa ikiwa kuwa na nidhamu katika usimamiaji wa miradi yote ya Serikali inayoletwa.
“Fedha za umma siyo za mtu binafsi unapozitumia lazima zitumike kwa mujibu wa Sheria,asitokee mtu akajimilikisha atatuangusha, tunayo Hospitali na Shule tukasimamie iishe ili tuombe fedha kwaajili ya miradi mingine”.
Mgema amesema Serikali imeleta milioni 470 kwaajili ya ujenzi wa Shule na Hospitali hivyo ametoa rai kwa watumishi na Madiwani kusimamia miradi hiyo na kuhakikisha inakamilika kwa wakati .
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Teofanes Mlelwa katika kikao hicho ametoa rai kwa watumishi wa Halmashauri hiyo kila mmoja kufanya kazi yake kwa weledi bila kusukumwa na kushirikiana kwa umoja ili kuhakikisha Madaba inasonga mbele.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma
Mei 19,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.