Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma imetoa mikopo kwa Vikundi 39 vya wajasiriamali Wanawake vikundi 17, watu wenye Ulemavu Vikundi 11 na Vijana vikundi 11 yenye thamani ya Shilingi 189,831,500 ikiwa ni asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri.
Hafla ya kuwakabidhi wanakikundi hao imefanyika, katika Ukumbi wa Jengo la Utawala,Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa, na mgeni rasmi katika Hafla hiyo ni Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mhe. Peres Magiri.
Akizungumza kabla ya kukabidhi Mikopo kwa wanakikundi hao, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mhe. Magiri, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, kwa kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Ndani, na kutoa mikopo kwa wajasiriamali , kwa lengo la kuongeza kipato kwa jamii.
Amewataka wanakikundi waliopokea fedha hizo kwenda kujiimarisha kiuchumi kwa kuongeza kipato na hatimaye kulipa deni hilo kwa kuwa Serikali imetoa fedha bila riba.
“Fedha hizi ni za mikopo hivyo basi wajasiriamali mnatakiwa kuongeza kipato na kurudisha mkopo ili na wengine waweze kupata mikopo hiyo awamu Nyingine”
Naye Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya ameishukuru Serikali inayoongozwa kwa kuwapa mikopo wananchi wa Jimbo la Nyasa, ili waweze kuongeza kipato zaidi na kuwataka wananchi kuendesha biashara zao ili wapate faida na kurudisha mikopo hii.
Manyanya ametahadharisha kwa waliopokea mikopo kuwa, mikopo hii sio zawadi hivyo wajitahidi kulipa ili na vikundi vingine vingine viweze kukopeshwa.
Awali akitoa taarifa fupi Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Nyasa, Khalid Khalif amesema Halmashauri ya Nyasa imetekeleza takwa la kisheria kwa kutoa mikopo hiyo kwa kuwa ilipokea maombi 133 na kuyachakata kutokana na ufuatiliaji uliofanyika vikundi 39 vimepata mkopo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.