• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

HAYUPO wa kuvuruga uchaguzi,Tiki kubwa kwa Samia-Wasira

Imewekwa kuanzia tarehe: June 10th, 2025

Katika hekaheka za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, ujumbe mmoja umesimama imara kama mnara wa taa katika giza nene ni ule alioutoa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira, akiwa katika  wilaya ya Tunduru, Mkoa wa Ruvuma.

 Katika kikao cha ndani kilichowakutanisha wanachama wa CCM, viongozi wa dini, na makundi mbalimbali ya kijamii, Wasira hakuacha shaka: “Watanzania, jiandaeni kutiki. Tiki kubwa kabisa kwa Rais Samia Suluhu Hassan na mgombea mwenza wake, Dk. Emmanuel Nchimbi.”

Katika ulimwengu wa siasa unaotikiswa na kauli tata kama "No Reform No Election", Wasira ameweka  wazi kuwa hakuna kikundi, mtu, wala kaulimbiu inayoweza kuzuia uchaguzi wa kidemokrasia nchini Tanzania.

Samia: Kiongozi wa Maridhiano

Wasira hakusita kumwelezea Rais Samia kama chombo cha maridhiano kilichosafisha njia ya maelewano miongoni mwa vyama vya siasa nchini.

Amesema Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake,Rais Samia amejitahidi kusikiliza kila upande hata wale waliotaka kusikika wao tu.

 “Hata CHADEMA waliposita, Rais Samia aliwasikiliza. Haya si maneno, ni historia ya kweli,” alisema Wasira kwa msisitizo.

Kauli hiyo iliambatana na mfano halisi wa matukio: “Juzi tu Mnyika alienda Kondoa kuhubiri ‘No Reform No Election’. Lakini wananchi wakamwambia macho macho tunaenda kutiki Oktoba.” Kwa maneno hayo, Wasira aligeuza sintofahamu kuwa uamuzi thabiti wa wananchi kuitikia wito wa uchaguzi kwa ari.

Uongo ni Giza, Ukweli ni Umeme

Wasira, mwanasiasa mwenye uzoefu wa miongo kadhaa, alitumia taswira nzito kuelezea mapambano kati ya propaganda na ukweli: “Uongo unafanana na giza, na ukweli unaogopwa na uongo kama vile giza linavyoogopa umeme.

 Aliongeza kuwa kazi ya viongozi ni kuwasha umeme huo kwa wananchi kwa kuwapa elimu, uelewa na hamasa ya kushiriki uchaguzi.

Tanzania: Nchi ya Amani na Umoja wa Kweli

Katika kipengele kilichogusa mioyo ya wengi, Wasira alisisitiza kuwa Tanzania ni nchi ya nadra barani Afrika nchi inayosimama kwa amani, umoja na mshikamano. Alisema, “Afrika ina matatizo mengi, lakini Tanzania haijawahi kushuhudia mapinduzi ya kijeshi, vita vya wenyewe kwa wenyewe, wala machafuko ya kisiasa. Huu ni ushahidi wa kazi nzuri iliyofanywa na chama chetu na viongozi wake.”

Aliendelea kueleza kuwa dini si chanzo cha migogoro nchini. Kwa kutumia mfano wa Ibrahimu, chimbuko la dini zote kuu, alisema, “Ibrahim kasema tugombane? Hapana. Mungu mmoja ametuita tumwabudu, si tugombane.”

CCM: Chama Kilichojenga Msingi Imara

Kwa mujibu wa Wasira, tofauti ya CCM na vyama vingine iko wazi: ni chama kilichojenga msingi wa amani na maendeleo kwa miaka zaidi ya 60. “Hatutaki ugali wa jana kama kiporo, tunataka ugali wa moto unaotoa moshi maendeleo yanayoonekana, yanayogusa maisha ya watu.”

Alimnukuu Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete aliyewahi kusema, “Nchi haiwezi kupoa kama ugali wa jana,” akimaanisha kuwa maendeleo lazima yawe endelevu na yenye msukumo wa sasa.

Tiki Siyo Tena Alama—Ni Dhamira ya Taifa

Hotuba ya Wasira ni mwaliko wa kuchagua si tu wagombea, bali mustakabali wa taifa.Na kama alivyoeleza kwa sauti ya mwisho:“Msibabaishwe nenda mkapige kura. 


Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WAKULIMA Ruvuma waomba soko la mahindi kufunguliwa haraka

    June 16, 2025
  • SERIKALI ,dini na wananchi Ruvuma waungana kudumisha amani

    June 16, 2025
  • RUVUMA yaandika historia chupa 4040 za damu zakusanywa kuokoa maisha

    June 15, 2025
  • NAMTUMBO yaagizwa kuongeza kasi ya kushughulikia hoja za CAG

    June 15, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.