Na Albano Midelo
TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete inatarajia kuitumia Hospitali ya wilaya Namtumbo kama kituo kidogo cha uchunguzi wa Matibabu ya moyo ili kusaidia wananchi wenye hali ya chini mkoani Ruvuma kupata huduma karibu za matibabu.
Madaktari Bingwa kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) wamepiga kambi ya siku saba wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma kwa ajili ya kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa wilaya ya Namtumbo.
Akizindua huduma hizo Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Mheshimiwa Vita Kawawa amesema, zoezi la uchunguzi na matibabu ya moyo kwa wananchi litasaidia kuokoa maisha ya watu wengi ambao awali walishindwa kupata huduma hizo kutokana na gharama ya kufuata matibabu nje ya wilaya ya Namtumbo.
Kawawa,ameishukuru Serikali kupitia Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI),kwa kuleta Madaktari Bingwa watakaotoa huduma kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo,uzito mkubwa na shinikizo la damu.
Aidha Kawawa,ameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta zaidi ya Sh.bilioni 2.3 zilizosaidia kuboresha miundombinu ya Afya katika Hospitali ya wilaya Namtumbo.
Amesema,fedha hizo zimetumika kujenga jengo la huduma za meno, macho,jengo la mama ngojea na jengo la Mama,Baba na mtoto.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt Aaron Hyera amesema,uboresha wa miundombinu katika sekta ya afya uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita umesaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati na baada ya kujifungua.
Amesema uwekezaji wa miundombinu katika sekta ya afya wilayani humo umewezesha kutoa huduma kwa ubora zaidi hasa ikizingatiwa baadhi ya vijiji viko umbali wa zaidi ya kilometa 200 kutoka makao makuu ya wilaya Namtumbo mjini na vituo vya afya vilivyopo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.