Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amekutana na mpambanaji Selemani Kidunda na kumpongeza kwa kazi anayo ifanya.
Akizungumza ofisini kwake leo amewatakia heri vijana watano kutoka Jeshi la kujenga Taifa akiwemo mpiganaji Kidunda.
"Nitumie fulsa hii kukupongeza Selemani Kidunda kwa kulibeba Jeshi la wananchi Tanzania na kuliheshimisha pamoja na nchi yako”.
Ibuge ameahidi kuhudhuria shindano hilo litakalofanyika Julai 30,2022 na amewahamasisha wananchi wote wa Mkoa wa Ruvuma na Mikoa jirani kuhudhuria pambano hilo.
Rc amepongeza jitihada za makocha kwa kuendelea kuwafundisha wapambanaji pamoja na vijana watano watakao shiriki pambano hilo.
Imeandaliwa na Janeth Ndunguru
Kutoka Kitengo cha Mawasilianao Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Julai 26,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.