ALIYEKUWA Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Meja Jenerali Wibert Ibuge,amekabidhi ofisi kwa Mkuu wa mkoa huo Kanali Laban Thomas,makabidhiano yaliyofanyika katika ofisi za mkuu wa mkoa na kushuhudiwa na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Serikali.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo,Meja Jenerali Ibuge amempongeza Kanal Laban kwa kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa na amemtakia majukumu mema Kanal Laban katika majukumu mapya ya nafasi hiyo.
Ibuge alisema kuwa, hana shaka hata kidogo na mkuu huyo mpya kwa kuwa anaufahamu vyema mkoa wa Ruvuma wakati akiwa mkuu wa wilaya ya Nyasa.
“nawashukuru wananchi,watendaji na viongozi wote wa serikali ya mkoa wa Ruvuma kwa ushirikiano mlionipa wakati wote niliokuwa nanyi katika nafasi ya mkuu wa mkoa kwa muda wa mwaka mmoja na miezi miwili, sina shaka na Kanal Thomas kwani ana uzoefu mkubwa na anaufahamu mkoa huu”alisema Jenerali Ibuge.
Alisema,akiwa mkoani Ruvuma kama kiongozi namba moja alifurahi sana kufanya kazi na wakuu wa wilaya ambao walimsaidia kutekeleza majukumu yake kwa weledi na uaminifu mkubwa jambo lililosaidia mkoa huo kupiga hatua kubwa ya maendeleo.
Aidha Meja Jenerali Ibuge,amewashukuru waandishi wa Habari wa mkoa huo kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kuandika na kutangaza shughuli mbalimbali za maendeleo.
Alisema,vyombo vya Habari vilikuwa na mchango kubwa na kuwezesha mkoa huo kuwa miongoni mwa mikoa iliyopiga hatua kubwa ya kiuchumi na kuwa miongoni mwa mikoa inayochangia pato la Taifa kwa asilimia kubwa.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa huo Kanal Laban Thomsa,amempongeza Meja Jenerali Ibuge kwa kupandishwa cheo kutoka Brigedia Jenerali hadi Meja Jenerali.
Amehaidi kutoa ushirikiano kwa watendaji na viongozi wa ngazi mbalimbali za serikali katika mkoa huo huku akiwataka kwenda kusimamia zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika mwezi huu nchini kote
“ naomba sana viongozi wenzangu kwenda kuhamasisha wananchi kujiandaa na zoezi la sensa ambalo ni muhimu kwa manufaa ya nchi yetu”alisema Kanal Laban.
“Jenerali Ibuge,nitaendelea kuomba ushirikiano wako,na kujifunza ubunifu wako katika majukumu ya kumsaidia Mheshimiwa Rais kujenga nchi yetu”aliongeza Kanal Laban.
Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Mgema alisema,chini ya uongozi wa Jenerali Ibuge amejifunza mambo mengi mazuri ikiwamo suala la kujali muda kwa watumishi wa umma na usikivu kwa mtu yoyote bila kujali nafasi yake.
Alisema,tabia hiyo ni muhimu kwa kiongozi yoyote wa umma katika kuwatumikia wananchi.
Pia,amempongeza Jenerali Ibuge kwa kusimamia vema utekelezaji wa miradi ya maendeleo hasa sekta ya kilimo ambayo ni uti wa mgongo kwa wananchi wa mkoa huo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.