KAMISHNA wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Ruvuma Ildefonce Ndemela ameunga mkono katika kufanikisha utekelezeji wa Operesheni ya uwekaji wa anwani za makazi na postikodi.
Amesema katika kufanikisha mfumo huu sekta ya Ardhi itahakikisha kuwa inaandaa na kuziingiza kwenye mfumo taarifa zote za upangaji, upimaji na umilikishaji wa Ardhi.
Ndemela amesema kuwa sekta ya Ardhi ina majukumu mbalimbali katika kufanikisha zoezi hili ikiwemo kuboresha na kukamilisha taarifa za umiliki, kuandaa taarifa za michoro ya mipango miji na Ramani za upimaji pamoja na kuandaa Ramani za mipaka ya maeneo ya kiutawala.
Hata hivyo Ndemela ameongeza kuwa sekta ya Ardhi ina majukumu ya kubadilisha michoro ya Mipangomiji na Ramani za upimaji kutoka katika mfumo wa analojia kwenda katika mfumo wa kidigitali pamoja na kuandaa ramani na taarifa za vipande vya Ardhi kwenye maeneo yaliyoendelezwa kiholela.
‘’Ndugu zangu napenda kuwaambia kuwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika ngazi zote yaani Makao makuu, Ofisi za Ardhi Mkoa hadi Halmashauri tumejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa zoezi hili linakamilika ndani ya muda uliopangwa na kwa ubora uliokusudiwa’’ amesema
Kamishna wa Ardhi Msaidizi ametoa maelekezo kuwa faida ya taarifa za Ardhi katika zoezi hili ni kurahisisha ukusanyaji wa maduhuli mbalimbali ya Serikali ikiwemo kodi ya pango la Ardhi na ada zingine za Ardhi.
Imeandaliwa na Bahati Nyoni
Kutoka Ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Februari 16,2022
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.