Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jitegemee Holdings, Emmanuela Kaganda ambayo inamiliki mgodi wa Makaa ya mawe katika kijiji cha Ntunduwaro Kata ya Ruanda Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma amesema shughuli za uzalishaji katika mgodi zilianza rasmi Mei 2021 na una uwezo wa kuzalisha tani 2,500 hadi 3,000 za makaa ya mawe kwa siku kwa mashine zilizopo kwa sasa.
Hata hivyo amesema hadi kufikia Desemba 2022, jumla ya dani 652,128.8 za makaa ya mawe zimevunwa.
“Hadi kufikia Mwezi Desemba 2022 kampuni imeshauza jumla ya tani 522,450.08 za makaa ya mawe kwa wateja wa ndani na nje ya nchi.
Amesema Kampuni imefanikiwa kusafirisha makaa ya mawe meli moja ya tani 22 kwenda nchini Congo DRC na mwezi huu wa Januari 2023 kampuni itasafirisha meli mbili za makaa ya mawe kwenda nje ya nchi. Meli moja ya tani 25,000 tayari ipo bandari ya Mtwara itaelekea Congo DRC na meli ya pili imeshafika nayo inapakia tani 55,000 za makaa kuelekea nchini Polland.”
Amesema kampuni yao imefanikiwa kuchangia shilingi bilioni 7.01 katika pato la Taifa, kati yake shilingi milioni 81.73 zimelipwa kwa halmashauri kupitia tozo na ushuru mbalimbali na Shilingi Milioni 292 ni kodi nyingine za serikali ikiwemo PAYE, kodi ya zuio na SDL.
“Kampuni imeshalipa Mrabaha jumla ya kiasi cha Shilingi Bilioni 3.59 na shilingi milioni 488 kama ada ya vibali vya kusafirisha mkaa nje ya nchi kuanzia Juni 2021 hadi Disemba 2022.”
Mkurugenzi huyo alikuwa anatoa taarifa ya mgodi huo kwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa alipotembelea na kukagua mgodi huo.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amekipongeza kikundi cha Mbalawala Women group kilichopo Ruanda, Wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma ambacho kinajihusisha na utengenezaji wa mkaa wa kupikia kupitia makaa ya mawe na kwamba Serikali itaendelea kuwasaidia ili kuhakikisha wanaendelea na uzalishaji huo ambao ni muhimu katika utunzaji wa mazingira
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.