Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Ndugu. Stephen Mashauri Ndaki amewataka wataalamu wa Ardhi mkoani humo kutatua migogoro ya Ardhi kwa kuwatembelea Wananchi katika maeneo yao badala ya migogoro hiyo kuwafuata ofisini
Maagizo hayo yametolewa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Ndugu. Jeremiah Sendoro. kwenye kikao cha watumishi wa Sekta ya Ardhi Mkoa wa Ruvuma,kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea Machi 21,2023.
Ndaki amesema Serikali kupitia Wizara ya Ardhi imewapa dhamana kuhusu rasilimalia Aridhi lengo likiwa Wananchi kuwa na uhakika na usalama wa miliki zao za Aridhi na ili kuboresha huduma hiyo lazima kuwe na mfumo rahisi pamoja na kusogeza huduma kwa Wananchi
“Ndugu wa wataalamu kwa kuwa adhima kuu ya Serikali ya kusogeza ofisi karibu na Wananchi ni kupunguza au kuondoa adha kwa wananchi kufuata huduma hii mbali,” amesema Ndaki
Hata hivyo ametoa maelekezo kwa watalaamu ao amewataka kuhakikisha kila mtaalamu ya sekta ya Aridhi anatekeleza majikumu yake na pia kwa kuzingatia maadili ya kazi na weledi pamoja na kutojiusisha kuomba na kupokea rushwa yoyote na kuhakikisha wanatunza vyema nyaraka za Serikali
“Katika hili naelekeza kila Halmashauri iweke utaratibu wa kufanya mikutano ya hadhara katika mitaa ili kutoa elimu kwa Wananchi kuhusu sheria mbalimbali zinazotawala maswala ya Aridhi ili Wananchi waweze kutambua wajibu wao,” amesisitiza Ndaki
Naye Kamishna wa Aridhi Msaidizi Mkoa wa Ruvuma Ndugu Idefonce Ndemela amesema idara ya utawala ya Aridhi imeendelea kuhamasisha kushirikiana na Hamashauri hadi kufukia Machi 16,2023 Mkoa wa Ruvuma umekusanya kiasi cha shilingi bilioni 1.2 ambayo ni sawa na asilimia 42.3 lengo likiwa kukusanya bilioni 3 kwa mwaka
Ndemela amesema pamoja na jitihada za ofisi ya Aridhi ikiwa inafanya kwa ajili ya kutekeleza malengo ya Wizara ikiwemo kuongeza ukusanyaji wa kodi wa Ardhi kuna changamoto mbalimbali ambapo kutokuwa na usafiri kwa baadhi ya Halmashauri kwa ajili ya kufanya kazi zao za kila siku
“Lakini kiukweli taasisi za Serikali ndio zinaongoza kwa kulimbikiza madeni sisi kazi yetu ni kuwakumbusha kwa kuwapa taarifa ya kulipia ila jukumu la kulipa linabaki kwa taasisi husika tuanomba kupitia ofisi yako tusaidie katika hili,” amesema Ndemela.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.