Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma imepokea kifaa cha kisasa cha kuongeza virutubisho kwenye unga wa chakula kutoka Shirika la Sanku – Project Healthy Children, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha lishe kwa wananchi.
Kifaa hicho kimekabidhiwa rasmi katika ofisi za halmashauri na kinalenga kusaidia mashine za kusaga nafaka kuongeza virutubisho muhimu katika unga unaotumiwa na jamii.
Kifaa hicho kitawekwa kwenye moja ya mashine za kusaga mahindi katika kiwanda kidogo cha kusaga unga kilichopo ndani ya halmashauri hiyo, na kitakuwa na jukumu la kuongeza virutubisho muhimu kwa afya ya mama na mtoto.
Teknolojia hii inalenga kupunguza hali ya utapiamlo na udumavu kwa watoto wachanga.
Akizungumza wakati wa makabidhiano kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Madaba, Katibu wa Afya wa Wilaya hiyo Gabriel Kirigiti ameishukuru serikali pamoja na wadau kwa msaada huo muhimu.
Amesema kifaa hicho kitachangia kwa kiasi kikubwa kuboresha lishe na afya za wakazi wa halmashauri hiyo na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.