Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea, Dr. Magafu Majura amesema kuwa wanatarajia kupokea jopo la madaktari bingwa kutoka Hospitali za Rufaa za mikoa ya nyanda za juu kusini ambayo Ruvuma, Njombe, Mbeya na Songwe.
Akizungumza ofisini kwake amesema kuwa wanatarajia kupokea madaktari bingwa ambao watatoa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea (HOMSO).
Dr.Majura amesema katika kambi hiyo kutatolewa huduma mbalimbali za kibingwa za akina mama na uzazi, huduma za magonjwa ya watoto, huduma za kibingwa za magonjwa ya ndani kama vile kisukari, shinikizo la damu, figo na moyo, huduma za upasuaji na mifupa, huduma za macho, huduma za Afya ya akili, huduma za kinywa na meno, huduma za masikio, pua na koo, huduma za ngozi, huduma za mfumo wa chakula, huduma za moyo kwa watoto, huduma za saratani.
“Kutokana na uhaba wa huduma hizo Wananchi wamekuwa wakisumbuka kufuata matibabu ya kibingwa mbali hivyo Serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na uongozi wa Mkoa wa Ruvuma imesogeza huduma karibu ili kuondoa usumbufu kwa Wananchi” amesema Dr. Majura
Amesema ujio wa madaktari hao utakuwa ni fursa kwa wataalamu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea (HOMSO) kwa sababu watawajengea uwezo wataalamu waliopo.
Dr. Majura amewahimiza wananchi kufika na kupata huduma na kwamba kutakuwepo na wataalamu wa huduma za mionzi za damu za usingizi na ganzi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.