MSIMAMIZI wa Uchaguzi Jimbo la Madaba wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Sajidu Idrisa Mohamed amefunga mafunzo ya Makarani yaliyofanyika kwa siku moja ambapo amewaagiza makarani hao kuzingatia yote yaliyofundishwa.
Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba amewapongeza wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Jimbo pamoja na Maafisa kutoka Tume ya Uchaguzi kwa ushirikiano ulioonyeshwa kwaajili ya kutoa mafunzo hayo kwa Makarani.
“Mkasimamie zoezi la uchaguzi kwa weledi kama mlivyofundishwa pamoja na kuwa makini katika zozi hili la Kitaifa tutangulize Maslahi ya Taifa Mbele”.
Hata hivyo amesema Makarani hao watakapo kuwa katika eneo la kituo cha uchaguzi wazingatie kuwa nadhifu pamoja na kujiamini kupitia maarifa waliyo patiwa na wasimamizi wasaidizi wa Jimbo.
“Najua asubuhi mmekula kiapo cha kujitoa uanachama na kutunza Siri tunaamini mtaenda kujiamini pamoja na kuwa na Lugha ya staha kwa wapiga kura”.
Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zakia Mohamed Abubakari mara baada ya mafunzo hayo kumalizika amewapongeza Makarani waongoza wapiga kura kwa mafunzo usikivu na uelewa wa haraka.
Hivyo Kamishna amesisitiza kuwapa kipaumbele wenye mahitaji maalum na kutojisahau wanapokuwa katika kituo cha uchaguzi
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.